PEACE

KARIBU TANZANIA/ WELCOME TO TANZANIA

Saturday, April 25, 2009

DECI watoka kapa

Wanachama wa taasisi ya DECI inayowezesha watu kupanda na kuvuna mapesa kwa faida nono wamegonga mwamba leo baada ya zoezi la ulipaji wa fedha zao walizopanda kama mbegu kutofanyika.

Awali, wanachama hao walikuwa wakitarajia kuanza kung\'oa `mbegu` zao leo, hasa baada ya kutangaziwa ratiba ya kufanya hivyo na uongozi wa taasisi hiyo yenye makao yake makuu pale Mabibo Mwisho Jijini.

Wakizungumza katika ofisi za Alasiri leo asubuhi, baadhi ya wanachama hao wa DECI wamesema kuwa uongozi wa taasisi hiyo (DECI) umewageuka leo asubuhi, kwani badala ya kuanza kuwalipa pesa zao kama walivyoahidi kupitia ratiba yao, wamekuta tangazo linalowaambia kuwa hawatalipwa kwa sababu akaunti za taasisi hiyo zimefungiwa na Serikali.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, kiongozi wa wateja hao walio katika tawi la Kinondoni Jijini, Bw. James Owe Risso, amesema kufuatana na ratiba iliyotolewa awali na uongozi wa kampuni hiyo Jumanne iliyopita, ni kwamba wateja 236 wa tawi hilo la Kinondoni walitakiwa kung\'`oa mbegu zao leo.

Akasema hadi jana jioni walipoondoka katika ofisi hizo, waliambiwa kwamba leo wangeng`oa mbegu zao, jambo ambalo liliwafanya wadamkie katika ofisi hizo na wengine kukesha ili kuwahi foleni.

``Tumefika pale tukakutana na tangazo ambalo halikuwa na muhuri wala nembo likisema kuwa leo hatutaweza kung\'oa mbegu zetu kwa sababu serikali imefungia akaunti,`` akasema.

Akaongeza kuwa kwa jinsi lilivyokuwa, yeye na baadhi ya wanachama wenzie hawakuliamini tangazo hilo.

Akasema ilipofika mishale ya saa 2:30 leo asubuhi, baadhi ya wafanyakazi wa DECI walifika katika ofisi hizo za Kinondoni na kuwatangazia kuwa wasingeweza kung`oa mbegu zao kwa sababu akaunti zimefungiwa na Serikali.

``Tukawahoji hiyo Serikali imefungia jana usiku ama leo asubuhi? Maana hadi walituambia kuwa tungeng\'oa mbegu leo,`` akasema.

``Swali hilo hakuna aliyeweza kutujibu,`` akaongeza.
Akasema wanashangaa kwanini ofisi hizo zinaendelea na shughuli za kuwasajili wateja kwa ahadi ya kuwalipa fedha zao wakati wakijua wazi kuwa akaunti zao zimefungiwa.

Wateja hao wakaiomba serikali kuwaeleza ni lini watalipwa fedha zao na pia kusimamia zoezi hilo kutokana na ukweli kuwa taasisi hiyo inatia shaka katika kukamilisha zoezi la kuwasajili.

Aidha, akasema katika zoezi hilo, tofauti na wenzao wa matawi mengine, wao wakienda kujiorodhesha wamekuwa wakitakiwa kuacha risiti zao kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Aidha, wamedai baadhi ya wateja wamekuwa wakigongeshewa mhuri unaoonyesha kuwa wamelipwa na kwamba wameshapokea fedha zao.

Hivi karibuni, Serikali ambayo inaendelea kuichunguza DECI, ilitangaza kufungia akaunti za taasisi hiyo na pia za baadhi ya wakurugenzi wake ili kuhakikisha kuwa watu waliopanda pesa zao wanarejeshewa.

1 comment:

Anonymous said...

Good day, sun shines!
There have were times of troubles when I felt unhappy missing knowledge about opportunities of getting high yields on investments. I was a dump and downright pessimistic person.
I have never thought that there weren't any need in large starting capital.
Now, I'm happy and lucky , I started take up real money.
It gets down to select a correct partner who uses your money in a right way - that is incorporate it in real business, and shares the profit with me.

You may get interested, if there are such firms? I have to tell the truth, YES, there are. Please get to know about one of them:
http://theinvestblog.com [url=http://theinvestblog.com]Online Investment Blog[/url]