PEACE

KARIBU TANZANIA/ WELCOME TO TANZANIA

Sunday, August 24, 2008

Idadi ya samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria inazidi kupungua-Magufuli

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa John Magufuli amesema idadi ya samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria inazidi kupungua kutokana na uvuvi haramu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza amesema idadi ya sangara katika ziwa hilo imepungua kutoka tani 750,000 mwaka jana hadi kufikia tani 350,000 Februari mwaka huu. Kwa mujibu wa Mheshimiwa Magufuli kutokana kutokana na hali hiyo serikali imeanza kusimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni nyingine ili kudhibiti uvuvi haramu wa kutumia makokoro, sumu na nyavu zisizoruhusiwa. Aidha amewataka amewataka maafisa uvuvi nchini kusimamia kikamilifu waraka uliotolewa na wizara yake kudhibiti uvuvi haramu ili kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la taifa. Amebainisha kuwa mchango wa sekta ya uvuvi katika pato ni asilimia 1.3 tu wakati nchi nyingine kama Namibia mchango wa sekta hiyo ni asilimia 23.

No comments: